Staa wa Bongo fleva, Kassim Mganga amesema hapendezwi na tabia za baadhi ya wasanii ambao wanawadanganya mashabiki kwa kusema wanamiliki  vitu vya thamani ambapo siyo kweli.

Staa huyo amesema wasanii wengi wa bongo wanaigiza maisha ili kuwadanganya watu na kujilinganisha na wasanii wa Marekani ambao hizo mali zinakuwa ni zao kweli.

Kassim Mganga amesema kitu ambacho amejifunza  kuwa wasanii wenzao wa Marekani awaigizi maisha ndiyo wanavyoishi kweli tofauti na baadhi ya wasanii wa hapa Bongo

Pia staa huyo aliendelea kwa kusema kuwa kitendo hicho si kizuri hasa kwa wasanii wachanga ingawa hakuna mtu anayekatazwa ku’post kitu kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wasanii wamekuwa wakikerwa na tabia ya wasanii wenzao ambao wanaigiza maisha ambayo siyo halisi ambapo ukiachia Kassim Mganga kusema hivyo Msanii Nikki wa pili nae alishawahi kusema hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *