Golikipa wa Leicester City, Kasper Schmeichel amerejelea mazoezi katika klabu yake baada ya kupona majeruhi ya mkono aliyoyapata mwezi Novemba mwaka huu.

Kuna uwezekano huenda akaweza kucheza mechi ya Jumamosi ugenini dhidi ya Stoke City kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Schmeichel mwenye miaka 30 aliumia mkono wa kulia wakati wa mechi yao Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen tarehe 2 Novemba ambayo ilimalizika kwa sare ya bila bila.

Leicester wameshinda mechi mbili pekee kati ya nane walizocheza kwenye ligi na katika michuano ya kombe la ligi tangu wakati huo.

Schmeichel amechezea Leicester mechi 38 za ligi msimu uliopita na kumaliza mechi 15 kati ya hizo bila kufungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *