Golikipa wa zamani wa klabu ya Simba SC, Juma kaseja ameteuliwa kukaimu kwa muda nafasi ya kocha msaidizi wa Serengeti boys katika kambi itakayowekwa nchini Madagascar pamoja na mchezo dhidi ya Afrika kusini.

Taarifa ya kuteuliwa kwa Kaseja kukaimu nafasi hiyo imethibitishwa na Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini “TFF”, Alfred Lucas katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Golikipa huyo mbali na kuwa msaidizi wa Kocha Bakar Shime, Kaseja atakuwa pia ni kocha wa makipa kwenye kikosi hiko.

Kikosi cha Serengeti Boys kimeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Madagascar kwa ajili ya kuendelea na kambi ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana dhidi ya Afrika kusini utakaochezwa mwezi ujao.

Jumla ya wachezaji 19 ndio watakaoelekea Madagascar wakiongozwa na Meneja wa timu Ayubu Nyenzi, Kocha mkuu Bakari Shime, daktari wa timu Sheikh Ngazija, pamoja na mtunza vifaa Andrew Andrew.

Serengeti Boys: Kikosi cha wachezaji wa Serengeti boys
Serengeti Boys: Kikosi cha wachezaji wa Serengeti Boys

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *