Staa wa Hip Hop nchini Marekani, Kanye West ametimiza ahadi yake aliyoitoa Novemba mwaka jana ya kuwagawia viatu vya Adidas mtindo wa Yeezy (Yeezy Boosts) wapiga picha ambavyo yeye ndiye mbunifu.

Mwezi Novemba mwaka jana Kanye West aliwaambia wapiga picha hao kwamba ipo siku atawagawia viatu vya Yeezy mwakani ambapo ndiyo mwaka huu.

boot

Wapiga picha hao wameonesha kufurahishwa na kitendo cha West kuwazawadia Yeezy Boosts huku wakimpongeza West na mkewe Kim Kardashian kwa moyo huo wa kuwasadia huku wengine wakisema imekuwa ni neema ya Krismasi.

Jack Arshakyan ambaye ni mpiga picha aliyebahatika kupata zawadi hiyo aliandika maneno yafuatayo kwenye ukurasa wake wa Instagram,”Shukrani nyingi ziende kwenu Kim Kardashian na Kanye West kwa kutuzawadia mimi na mapaparazi wenzangu Yeezy Boosts 350″.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *