Staa wa hop hop nchini Marekani, Kanye West amekutana na kufanya mazungumzo na  rais mteule wa Marekani Donald Trump jijini New York.

Rais huyo mteule wa taifa kubwa dunia amesema kuwa walizungumza kuhusu maisha kabla ya kupigwa picha pamoja na mkali huyo wa hip hop nchini Marekani.

Trump amesema wawili hao ni marafiki na akamweleza Kanye kuwa mtu mzuri lakini hakusema iwapo mwanamuziki huyo atatumbuiza wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake mwezi Januari mwakani.

Taarifa kutoka Marekani zinasema Trump huenda anakabiliwa na tatizo katika kutafuta wanamuziki mashuhuri wa kutumbuiza siku ya kuapishwa kwake.

Kanye amekuwa akipumzika na kupata nafuu kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata mwezi jana.

Mwaka uliopita, Kanye alitangaza kwamba anakusudia kuwania urais mwaka 2020.

Lakini hivi majuzi amesema iwapo angepiga kura uchaguzi wa mwaka huu basi angempigia Donald Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *