Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na na Instagram ambazo zilikuwa na followers milioni 10.

Sababu za kufuta akaunti hizo hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema.

Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.

Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.

Kanye West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.

Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *