Mwanamuziki maarufu wa Marekani, Kanye West amesema kuwa nia yake ya kugombea urais wa Marekani mwaka 2020 ipo pale pale.

Kauli hiyo ya Kanye West imekuja baada ya Donald Trump kuchaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani pamekuwa na maswali ya je rapa Kanye West atatekeleza ahadi yake ya kugombania urais mwaka 2020.

Kanye West amesema “Napoongelea kuwa kwenye siasa simaanishi kuwa na mawazo ya siasa ila mimi naangali ubinadamu zaidi, watu na ukweli, kama kuna kitu naweza kufanya na muda wangu ndani ya siku moja kuleta tofauti kwa watu nikiwa hai basi nitajaribu ”.

Kanye West aliahidi kugombania urais wa Marekani mwaka 2020 baada ya kumalizika kwa muhula wa kwanza wa rais wa 45 Donald Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *