Kanda za maonyesho wa gwiji wa muziki wa Reggae Bob Marley ambazo ziliokotwa baada ya miaka 40 kwenye hoteli iliyotelekezwa jijini London zimetengezwa.

Kanda hizo halisi, zenye ubora wa juu wa kurekodiwa wakati alipokuwa anafanya maonyesho wa moja kwa moja kwenye miji ya London na Paris kati ya mwaka 1974 na 1978.

Kwenye kanda hizo, zinasikika vizuri nyimbo mbalimbali zikiwemo No Woman No Cry, Jamming na Exodus.

Mwanzoni iliaminika kuwa kanda hizo zilikuwa zimeharibika kiasi ambacho zisingetengenezeka tena hususani kutokana na uharibifu wa maji.

Bob Marley ambaye amngetimiza miaka 72 siku ya leo alifariki mwaka 1981.

Knda hizo ziliokotwa kwenye sehemu ya kupaki magari ya hoteli ya Kensal Rise, kaskazini-magharbi mwa London ambapo Bob Marley na kundi la Wailers walikaa wakati wa ziara yao ya Ulaya kwenye miaka ya katikati ya 1970.

Kanda hizo zilipatikana baada ya shabiki wa Marley na mfanyabiashara wa Uingereza Joe Gatt, alipopigiwa simu na rafiki yake aliyeziokota kwenye hoteli hiyo chakavu.

Kazi ya kuzitengeneza na kuzirudishia ubora wake imechukua mwaka mmoja na kugharimu £25,000 (TZS70m).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *