Viongozi wa Kampuni ya Kubashiri ya SporPesa yenye makao yake makuu nchini Kenya wamekutana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa mazungumzo ya kuwekeza kwenye soka nchini humo.

Viongozi wa Kampuni hiyo wakiongozwa na CEO, Pavel Slavkov wa Kampuni hiyo wamekutana Ikulu jijini Kampala kwa mazungumzo hayo na kumkabidhi Rais Musevani jezi na mpira.

Kampuni ya SportPesa mpaka sasa imewekeza kwenye nchi nne ambazo ni Tanzania, Kenya, Uingereza na Italia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *