Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu, SportPesa inayodhamini ligi kuu nchini Kenya imetia saini mkataba wa kuidhamini klabu ya Hull City inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Kampuni hiyo ambayo inaandaa mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi nchini Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini klabu hiyo kwa misimu mitatu.

Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao baada ya kufanikiwa kupanda daraja na mechi yao ya kufungua ligi watacheza dhidi ya mabingwa watetezi Leicester City.

Hully City: Wakishangilia moja ya magoli yaoHully City: Wakishangilia moja ya magoli yao

Udhamini wa SportPesa ndio wa juu zaidi kuwahi kupokelewa na klabu hiyo katika historia yake ya miaka 112 toka kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Kabla ya udhamini huo Hull City ilikuwa ikidhaminiwa na kituo cha burudani cha Flamingo Land.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *