Kampuni ya Google imepigwa faini ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya kampuni hiyo kukiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.
Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.
Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi.
Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.
Tume hiyo ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya Google tangu mwaka 2010
Mbunifu wa Android azindua simu mpya
Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.