Mahakama Kuu nchini Uganda imemrudisha gerezani msomi na mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni, Stella Nyanzi.

Stella Nyanzi mhadhiri na mtafiti wa chuo kikuu ametiwa gerezani zaidi ya wiki mbili zilizopita wakati nchi hiyo ilipomfungulia mashtaka kuhusiana na makosa ya mtandaoni.

Makosa hayo yanatokana taarifa alizoweka kwenye mtandao wake mashuhuri wa facebook ambapo amewashutumu Museveni na mke wake kwa kuvunja ahadi ya uchaguzi ya kutowa vitaulo vya wanawake vya kujistiri wakati wa kupata siku zao.

Mke wa Museveni ni waziri wa elimu nchini Uganda. Msomi  huyo alikuwa amefikishwa mahakama kuu kuomba dhamana baada mahakama moja ya chini kukataa kusikiliza kesi hiyo.

Pia alikuwa akitaka mahakama hiyo kuu kuacha kuzingatia ombi la serikali la kutaka afanyiwe uchunguzi wa akili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *