Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Bw. Alphayo Kidata anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Peter Ilomo ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Alphayo Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Uteuzi wa Bw. Alphayo Kidata unaanza mara moja na ataapishwa kesho tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *