Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeanza kumuhoji Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wito wa kufika mbele ya kamati hiyo umefikiwa kufuatia azimio la Bunge kumuomba Mhe Spika kuwaita mbele ya kamati wakuu wa wilaya na mikoa waliotoa matamshi ya kudharau mamlaka ya Bunge.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Alexzender Mnyeti kwa kosa la kulidharau Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mahujiano ya Mkuu wa Mkoa huyo yameanza kufanyika jana mkoani Dodoma mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *