Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa jumla ya watuhumiwa 349 wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya toka kuanza kwa operesheni ya kudhibiti madawa hayo Februari 1 mwaka huu.

Katika watuhumiwa hao jumla ya watuhumiwa 16 wamefikishwa mahakamani kutokana na makosa hayo na majarada ya watuhumiwa 24 yapo kwa wakali wa serikali kuhusu kesi hiyo.

Sirro amesema kuwa Agnes Masogange ni miongoni mwa watuhumiwa hao ambapo amepelekwa kwa mkemia mkuu kupimwa kama anatumia dawa za kulevya na kama vipimo vikibaini anatumia kesho atapandishwa mahakamani.

Pia Kamanda Sirro amesema kuwa jeshi hilo limemkamata kijana mmoja Omar Abed Bakari ambaye alisambaza karatasi iliyokuwa na majina batili ya orodha ya mkuu wa mkoa ambaye alimkabidhi kamishna mkuu wa kupambana na dawa za kulevya.

Kwa upande mwingine kamanda Sirro amesema kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amefikshwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili za matumizi ya dawa za kulevya baada ya kubainika kutumia dawa hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *