Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametoa rai kwa wakazi wa jiji hilo na wageni wanaoingia jijini humo kutoka katika mikoa mbalimbali kupuuza taarifa za sauti zinazosambazwa kwenye mitandao ya jamii kuwa polisi wanawakamata hovyo wanaolala mchana kwenye nyumba za wageni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sirro kuwa habari zinazosambazwa katika mitandao ya WhatsApp naTelegram, pamoja na zilizochapishwa kwenye baadhi ya magazeti kuwa polisi wanawakamata watu hao kwa madai ya uzururaji na uzembe ni uvumi.
Kamanda Sirro alisema kwa nia ovu, taarifa hizo zimedai kuwa hatua hiyo ni kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la ‘Hapa Kazi Tu’, jambo ambalo si la kweli.

Amesema katika taarifa yake hiyo kuwa uchunguzi umebaini kuwepo na nyumba za kulala wageni zinazoendesha biashara kiholela kwa kuhifadhi wahalifu, wakiwemo wanawake na wanaume wanaouza miili yao.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *