Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kuwa mkuu wa jeshi la Polisi nchini.

Uteuzi wa Sirro umekuja kufuatia mkuu jeshi la Polisi nchini IGP, Ernest Mangu uteuzi wake kutenguliwa jana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inasema kuwa Ernest Mangu atapangiwa kazi nyingine hapo baadae.

Kamishana Sirro anatarajiwa kuapishwa leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *