PolisiΒ Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imemtaka yeyote anayeona kuwa kauli iliyotolewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako imetishia maisha yake afungue kesi.
Kamanda Simon Sirro ameyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatua polisi waliyoichukua kutokana na kauli aliyoitoa Mchungaji huyo kwamba waandishi waliomwandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani.
Β
Kauli ya Mzee wa Upako aliitoa katika mahubiri yake ya Jumapili ikiwa ni mwendelezo wa majibu yake kutokana na tuhuma zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba alimfanyia fujo jirani yake.