Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 10 ambao ni wakazi wa Kimara ambao wamefariki dunia juzi baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya gongo ambayo inahisiwa kuwa ilikua na sumu.

Watu hao waliofariki ni pamoja na Muhammed Issa(67)mkazi wa Kimara Saranga, Barubu Rashid (64) Stanlaus Joseph, Steven Isaya (61), Monica Rugurukama(42), Alex Madega(41), Hamis Mbara(35),Exson Nyoni (28) na Maleo Ramadhan.

Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa wamepata chupa 3 zenye ujazo wa lita moja aina ya gongo na vielelezo vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina gani ya sumu ilikuwa kwenye pombe hiyo ambayo imeua watu hao wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *