Mwanamuziki mongwe wa miondoko ya Hip-Hop nchini, Kalama Masoud “Kalapina” amesema kwamba watu wanaukubali wimbo mpya wa  Profesa Jay ambayo amechanganya hip hop na singeli lakini kwa upande wake amesema haikubali hata kidogo.

Kalapina amesema anaamini huu ulikuwa ni wakati muhimu zaidi kwa Profesa Jay kutoa nyimbo ya hip hop zaidi ili kuupa nguvu muziki huo ambao kwa sasa unaonekana kupoteza nguvu.

Kalapina amesema kuwa ameamua kurudi kwenye muziki rasmi kwa kutoa kazi nzuri za hip hop ili kurudisha heshima ya muziki wa huo uliopteza mwelekeo kwasasa nchini.

Vile vile Kalapina amesema kwa sasa walikuwa wanahitaji sana nguvu kubwa ya Profesa Jay katika muziki huu wa hip hop, hivyo yeye kutoa hip hop singeli si mbaya kwa watu wengine lakini kwa upande wake anaona kama si sawa, kwani muziki wa hip hop saizi unahitaji nguvu zaidi.

Ameongeza kwa kusema kitendo cha Profesa Jay kuchana kwenye singeli, amemezwa kwenye singeli, hivyo ile siyo Hip hop tena ni singele zaidi.

Kalapina amesema kwamba ameamua kurudi rasmi kwenye game ya muziki wa Hip-Hop ili kurudisha heshima ya muziki wa hip hop Tanzania ambayo inaonekana kupotea.

Kwasasa Kalapina anatamba na nyimbo yake mpya ya Hip-Hop inakwenda kwa jina la “Wasiohusika na Show”.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *