Mwanamuziki wa hip hop nchini, Kalama Masoud ‘Kalapina’ ambaye pia ni mwanaharakati wa kupambana na madawa ya kulevya amefunguka kuhusu hali ya sasa ya mwanamuziki Chid Benz.

Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka ‘sober house’, hivyo amemtaka kurudi na kuwasikiliza watu waliomsaidia ili asifikie pabaya.

Kalapina aliendelea kusema kuwa Chid Benz na Ray C ambaye pia ni muathirika na madawa ya kulevya, walipata wafadhili wa kuwapeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kurudia kitendo hicho.

Pia Kalapina amekanusha suala la kwamba walimtelekeza msanii huyo, kwani walikuwa wanakwenda kumtembelea na kumpelekea mahitaji yote muhimu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *