Mwanamuziki wa hip hop nchini, Kalapina amewataka watu waliomteka mwanamuziki mwenzake Roma wasijaribu kumteka yeye kwani wataambulia kipigo kutoka kwake.

Kalapina amesema hayo jana wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha Radio nchini kuhusu kitendo cha kutekwa Roma Mkatoliki.

Mwanamuziki huo amempa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.

Kalapina amesema kuwa “ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua.

Ameongeza kwa kusema kuwa Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa.

Pia amesema kuwa Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo pale pale “.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *