Mkali wa hip hop nchini, Kala Jeremiah amesema kuwa  hana mpango wa kuachia albamu mpya mwaka huu kutokana na albamu yake ya kwanza kuendelea kufanya vizuri.

Mwnamuziki huyo amesema kuwa albamu yake iliyopita bado inaendelea kufanya vizuri mpaka sasa tofauti na alivyotarajia kwa hiyo hawezi kutoa albam nyingine wakati ya kwanza bado inafanya vizuri.

Rapa huyo amesema albamu hiyo ya kwanza bado inaendelea kumpatia mashavu mbalimbali katika muziki wake kwa kuwa hiyo ni CV ambayo anatembea nayo katika maisha yake ya muziki.

Kala kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Wanandoto’ ambao aliutoa miezi miwili iliyopita lakini umeonekana kufanya vizuri mpaka sasa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *