Mwanamuziki wa hip hop nchini, Kala Jeremiah ametunukiwa cheti ya heshima na Shirika la Society Watch kutokana na wimbo wake ‘Wanandoto’ ambao unatetea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Kala amelishukuru shirika hilo huku akidai hatua hiyo ni nzuri katika muziki wake kutokana na jamii kutambua mchango wake katika suala zima la sanaa yake.

Baada ya kupewa cheti hiko Kala amesema   nyimbo ya ‘Wanandoto’ unaotetea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu. Hakika cheti hiki ni kitu kikubwa sana kwangu na kwa muziki wangu. Nanicheti changu cha kwanza kabisa. Heshima hii ni kubwa sana. Nasema asanteni sana,”.

Wanandoto ni wimbo ambao umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na runinga huku kupitia mtandao wa YouTube ukiangaliwa mara 223,547 kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Kala Jeremiah ni mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye ni zao la Bongo Stars Search (BSS) amepata umaarufu mkubwa kutokana na tungo zake kugusa jamii moja moja mbali na kupata cheti cha heshima Kala pia alishawi kutwaa tuzo tatu kwa pamoja kwenye tuzo za Kilimanjaro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *