Staa wa Bongo movie, Kajala Masanja amesema kwamba haendi gym ili kuongeza shape ya umbo lake kama baadhi ya watu wengi wanvyodhani bali ufanya mazoezi hayo ili kukabiliana na tatizo la moyo ambalo limeshika kasi nchini.

Staa huyo amesema kwamba kama shape tayari anayo kampa mungu kama nikuongeza kidogo tu ila anafanya mazoezi ili kuweka mwili wake safi uweze kukabiliana na magonjawa.

masanja

Kajala ameongeza kwa kusema kwamba alishauriwa na daktari kufanya mazoezi kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo kwahiyo daktari alimwambia hata kama anaendelea na dawa na mazoezi yanasaidia zaidi.

Muigizaji huyo ameachia filamu yake mpya mwezi uliopita inayoitwa “Sikitu” ivyo amewaomba mashabiki wake wamsapoti kwa kununua kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *