Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja ameshiriki katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku inayoendeshwa na Kampuni ya Biko.

Droo ya kwanza ya kuwania Sh Milioni 10 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki imempatia donge nono mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya na kuweka historia ya kuwa mtu wa kwanza kujinyakulia kitita hicho kutoka kwa mchezo wa bahati nasibu wa Biko.

Droo hiyo ilichezeshwa na msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo kushoto akichezesha droo kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo kushoto akichezesha droo kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.

Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba jumla ya washindi 2000 walipatikana katika zawadi mbalimbali, huku Mgaya yeye akiibuka kinara wa Sh Milioni 10.

Heaven amesema kwamba baada ya kupatikana kwa mteja huyo, taratibu za kumkabidhi hundi yake ya Sh Milioni 10 unaweka ili mteja huyo apate fedha zake haraka iwezekanavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *