Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka sababu iliyomfanya ashindwe kwenda kituo cha Polisi (Central) kumuangalia Wema Sepetu ambaye alishikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya.

Kajala amesema kuwa wakati Wema aliposhikiliwa kituoani hapo yeye alisafiri na hakuwepo jijini Dar es Salaam ndiyo sababu ya kushindwa kufika kituoni hapo kumuangalia muigizaji mwenzake.

Muigizaji huyo ameamua kuweka wazi sababu hiyo baada ya kupata lawama kibao kwanini ameshindwa kwenda kumuangalia Wema wakati kipindi cha nyuma alimsaidia kwenye kesi yake na Wema akatoa Shilingi milioni 13 ili asifungwe.

Kajala amesema kuwa ameshazoea kutukanwa na kulaumiwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na sababu tofauti lakini kwa hili wanamuonea kwa kuwa hakuwepo Dar es Salaam.

Wema Sepetu ni miongoni mwa mastaa na watu mbalimbali waliotajwa hivi karibuni na Makonda wakituhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ambapo Jumatano iliyopita alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na dada wawili wa kazi ambapo walitoka kwa dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *