Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Kajala Masanja amekanusha tetesi zilizosambaa kwamba amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Petit Man.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kajala amesema kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Petit Man zaidi ya urafikia tu kwani wameshaachana kitambo tu na sasa hivi Petit Man ni sehemu ya familia yake tu.

Kajala ameamua kufunga hayo baada ya tetesi kuzagaa kwamba wamerudiana na Petit Man kutokana na kuonekana wakiwa pamoja kwa muda mwingi kuliko siku za nyuma.

Kajala ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram

 Jamani i think this is too much sasa na mnavuka mipaka. ifike muda watu muwe mnatumia akili kufikiria mnavyotaka kusema. Hivi kama ulishakuaga na mahusiano na mtu na hayo mahusiano yakaisha So huruhusiwi kuongea nae?? Are you guys Owkay?? Hivi mnajua mchango wa Petit katika maisha yangu? Mnajua jinsi alivyonisaidia wakati niko katika kipindi kigumu cha jela? Au mnakua mnaongea tu ili mfurahishe watu…

Petit sasahivi ni part ya familia yangu na sio mambo ya mapenzi. Kwani mimi sijui kama ana mke na ana familia? Why watu mnakua na akili fupi sana za kufikiri….mimi siwezi kuwa na ugomvi na esma kwasababu ya petit…esma ni mke wake na wana mtoto na kila mtu anajua…na mimi nitaendelea kumchukulia petit kama ndugu na rafiki wa karibu kwasababu ya mchango na msaada wake katika maisha yangu. Sitoacha kuongea na petit kwa ajili ya ujinga wenu mnaosema…haitawahi kuja kutokea…sasa basi, i think am clear na tumeelewana kabisa…nyie ndo mnakuaga chanzo cha watu kugombana bila sababu..tafuteni kazi za kufanya… have a lovely evening.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *