Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda na Biashara, Dkt. Dalaly Peter Kafumu, makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vicky Kamata wamejiuzulu nyadhifa zao hizo leo.

Wabunge hao wamesema wamefanya uamuzi huo ili waweze kupata muda wa kutosha kuwatumikia wananchi majimboni mwao.

Aidha viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo.

Kafumu ni Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM) ambapo Vicky Kamata ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akiwakilisha wanawake wa Mkoa wa Geita.