Mbunifu wa mavazi nchini, Martini Kadinda amesema hawezi kumchagulia Wema Sepetu marafiki wa kuwa nao karibu na hawezi kujiingiza kwa lolote katika ugomvi wao.

Kadinda amesema ugomvi ambao unatokana na marafiki zake Wema unamshusha Wema kwa kuwa Wema ni mtu maarufu na ana jina kubwa hivyo alichokifanya ni kumzuia Wema kuweka ugomvi wake katika mitandao ya kijamii.

Pia Martin ameendelea kuwasihi mashabiki zake kuendelea kumpenda Wema na kazi zake ambazo anazifanya na siyo vinginevyo na pia wasimuhukumu Wema kwa mambo yanayoandikwa mitandaoni kwa kuwa hawajui chanzo chake.

Hivi karibuni Wema Sepetu aligombana na rafiki yake anayefahamika kwa jina la Muna baada ya Wema kumshtumu rafiki yake huyo ni mtu anayepeleka habari za uongo kwa mama yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *