Viungo wa Manchester United, Paul Pogba na Marouane Fellaini watakosekana kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la ligi (EFL Cup dhidi ya West Ham Utd siku ya jumatano.

 

Wachezaji hao walionyeshwa kadi za njano katika mchezo wa ligi ya England uliochezwa jana kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya West Ham Utd ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Fellaini na Pogba wamefanya makosa katika mchezo huo yamewasababishia wachezaji hao kufikisha kadi tano za njano kila mmoja, ambapo kisheria wanapaswa kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja wa michuano ambayo ipo chini ya chama cha soka nchini England FA.

Manchester United wataikaribisha West Ham katika hatua ya robo fainali baada ya kuwatoa Manchester City kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *