Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amekanusha tetesi za timu yake kususia hafla ya kupokea Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara jana
Kaburu amesema kuwa wao wapo nje ya mji wa Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya fainali yao dhidi ya Mbao FC.
Makamo mwenyekiti huyo amefafanua jambo hilo baada ya kuenea uvumi kuwa timu hiyo iligoma kwenda kupokea tuzo zao kama walivyofanya wachezaji wengine waliotajwa jana katika hafla iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amesema “Sisi tupo Dodoma tunajiandaa na maandalizi yetu ya mwisho ya fainali za FA dhidi ya wapinzani wetu Mbao FC na hatujaweza kutuma mwakilishi yeyote katika hafla hiyo kutokana na viongozi wote tupo huku.
Ameongeza kuwa ‘Tukirudi ndiyo tutajua cha kufanya kama tukienda kuchukua tuzo hizo tutawaambia lakini sasa hivi ni mapema kulisema hilo”.
Pia Kaburu amesema timu yake imejiandaa vizuri katika fainali hiyo ili waweze kuchukua ubingwa na kuweza kuwakalisha nchi katika mashindano ya kimataifa.