Kaburi la aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga maarufu kama Ivan Don limewekewa ulinzi ili watu wasiibe fedha alizozikwa nazo tajiri huyo.

Walinzi hao wameanza kazi hiyo baada ya kumalizika kwa mazishi yaliyofanyika kijijini kwa marehemu, Kayunga nje kidogo ya jiji la Kampala nchini Uganda ambapo amezikwa kwenye makaburi ya famalia yao.

Taarifa zilizosambaa mitandaoni zinasema kuwa walinzi hao wameingia mkataba wa miaka mitano kwa ajili ya kulinda kaburi hilo.

Wakati wa maziko ya tajiri huyo, rafiki zake ambao wanaunda kundi la Rich Gang ambao ni matajiri walimwaga pesa zaidi ya milioni 30 za kitanzania ndani ya kabuli hilo kama kumuenzi rafiki yao huo.

Ivan Ssemwanga amefariki dunia nchini Afrika Kusini baada ya kupata mshtuko wa moyo na kuangua akiwa nyumbani kwake nchini humo na kupelekwa hospitali ndipo umauti ukamkuta akiwa kwenye hosptitali hiyo.

Mazishi yake yalifanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Kayunga nje Kidogo ya jiji la Kampala nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *