Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila atasalia madarakani mpaka mwisho wa mwaka 2017 licha ya muhula wake kumalizika mwaka huu baada ya makubaliano na upinzani yaliyofanyika leo nchini humo.

Viongozi wa Upinzani nchini wamesema kuwa muafaka umeafikiwa na chama tawala kuhusiana ubadilishanaji madaraka.

Katika makubalianao hayo waziri mkuu mpya atachaguliwa kutoka upande wa upinzani na muafaka huo utaalindwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Etienne Tshi-sekedi.

Rais Kabila amekuwa madarakani kwa mihula miwili sawa na katiba ya taifa ambapo uchaguzi mkuu ulitakiwa kufanyika mwaka huu.

Baada ya Kabila kukataa kuachia madaraka hatua hiyo imesababisha maandamano makubwa katika barabara za miji ya taifa hilo.

Serikali imekubaliana na mapatano hayo ambayo upinzani umesema kuwa yatatiwa saini leo kama ilivyopangwa na viongozi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *