Huenda hii ikawa ndio couple pekee kwenye uwanja wa Bongo Fleva ambayo iko ‘OPEN’ na bado inaendelea kushamiri, ukiachilia couple ya Navy Kenzo.

Ingawa tofauti ya imani za dini kwa wawili hawa, Jux na Vanessa inaweza kuwa chanzo cha kusambaratika kwa couple hii endapo kila mmoja ataamua kuitetea na kuilinda imani yake lakini amini kuwa ipo sababu nyingine tofauti ambayo Vanessa Mdee ameiweka wazi inayoweza kuwasambaratisha wawili hawa.

Huwezi kuamini, sababu hiyo haihusiani kabisa na uaminifu lakini inaweza kuingizwa kwenye kundi hilo endapo ushahidi wa kimazingira unavyoweza kuchochea.

Sababu gani hiyo? KILONGA LONGA, ni simu ya mkononi na kwa mujibu wa Mdee, Jux amekuwa hasomeki kabisa kwenye suala la mawasiliano hususani kujibu meseji za Vee Money.

Na moja ya sababu kubwa za kuvunjika kwa mahusiano mengi baina ya wapenzi ni kukosekana kwa mawasiliano yenye afya.

Na mbaya zaidi, Vee Money anadai kuwa wakati mwingine jux hajibu meseji zake while anaonekana yuko active kwenye social media.

Kunani? Watadumu? Navy Kenzo kwa kuepuka lawama za aina hiyo, wanatumia simu moja, yaani ukimpigia Aika na akapokea Nahreel basi wewe ongea tu alichokuwa unataka kusema ‘usijiumeume’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *