Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jux amefunguka na kusema kuwa aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee ni mtu muhimu sana kwake ukiacha familia.

Jux amesema kuwa anampenda sana Vanessa kuliko msichana yeyote yule na ategemei kumuacha, hata familia yake inajua kuwa ana upendo mkubwa kwa Vanessa.

Mwanamuziki amesema kuwa akiwaga mbali na Vanessa huwaga asubuhi akiamka cha kwanza anaingiaga Instagram kumuangalia Vanesaa baada ya hapo ndo anampigia kwa sababu hawezi kumpigia simu bila kuangalia picha zake.

Kuhusu kupata mtoto, Jux alifunguka kwamba: “Sa’hivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo kwa sasa wa kujipanga kupata mtoto na mpenzi wangu pia mtoto wangu wa kwanza nataka nimuite jina la Karim na si jina jingine zaidi ya hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *