Klabu ya Juventus imeifunga Tottenham 2-1 kwenye mechi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi iliyofanyika katika uwanja wa Melbourne nchini Australia mapema leo.

Juventus ilipata magoli yake kupitia kwa mshambuliaji wake, Paulo Dyabala mnamo dakika ya 6 ya mchezo, huku goli la pili likifunga na na beki, Mehdi Benatia katika dakika ya 15 ya mchezo huo.

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Juventus wakiwa mbele kwa magoli hayo mawili, na goli la kufutia machozi la Tottenham limefungwa na kiungo wake, Elik Lamela katika dakika ya 67 ya mchezo.

Timu hizo zipo nchini Australia, huku Juventus wakijiandaa na ligi kuu nchini Italia na Tottenham ikijiandaa kwa ajili ya ligi kuu nchini Uingereza ambapo ligi zote zinatarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *