Juventus na Real Madrid kumaliza utata leo

0
284

Klabu za Real Madrid na Juventus leo zitakutana kwenye fainali ya klabu bingwa Ulaya itakayofanyika katika uwanja wa Cardif nchini Wales.

Kwa upande wa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anakabiliwa na kizungumkuti cha kuamua nani kati ya Gareth Bale na Isco atacheza katika fainali ya hiyo leo kutokana na waote kuwa fiti.

Bale hajacheza tangu 23 Aprili kutokana na kusumbuliwa na majeha ya muda mrefu lakini sasa yuko sawa kucheza mechi ya leo.

Isco ambaye alijaza pengo lake naye amekuwa akicheza vyema sana na amefunga mabao matano katika mechi nane walizocheza hivi karibuni.

Kwa upande wa kocha wa Juventus, Max Allegri amesema kuwa wachezaji wake wote wako sawa kucheza fainali ya leo kutokana na kutokuwa na majeruhi.

Kocha huyo aliwapumzisha wachezaji wake, Gianluigi Buffon, Giorgio Chellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic na Leonardo Bonucci kwenye mechi ya mwisho ya Juve katika Serie A dhidi ya Bologna Jumamosi iliyopita.

Gianluigi Buffon, 39, atakuwa nahodha wa Juve katika mechi hiyo itakayochezewa Cardiff ambapo kipa huyo hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Juventus wametinga hatua hiyo ya fainali baada ya kuwalaza Monaco 4-1 kwenye hatua ya nusu fainali.

Wao Real Madrid waliwatoa Atletico kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kwenye mechi ya za nusu fainali ya mashindano hayo.

LEAVE A REPLY