Kanda ya video inayomuonesha mwanamuziki nyota wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber akimpiga ngumi shabiki wake usoni imetolewa.

Mtu huyo anaonekana kupeleka mkono wake katika dirisha la gari ya Bieber ambapo anapigwa ngumi na kuwachwa akitoka damu mdomoni.

Kanda hiyo inaonekana kurekodiwa mjini Barcelona ambapo msanii huyo alikuwa akitumbuiza ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya muziki.

Shabiki huyo anaonekana kuingiza mkono katika dirisha la gari hilo na kujaribu kumshika Bieber wakati gari linapoondoka mkono unaonekana ukitoka katika dirisha hilo.

Shabiki huyo baadaye anarudi nyuma na kuisogelea kamera akiwa na damu katika meno yake na midomo.

Newsbeat imewasiliana na wawakilishi wa msanii huyo lakini haijapata tamko lolote kutoka kwao.

Mapema siku hiyo msanii huyo alipigwa picha akifanya zoezi na wachezaji wa Barcelona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *