Staa wa muziki nchini Marekani, Justin Bieber amekataa dola milioni 5 alizopewa ili atumbuize kwenye show ya chama cha Republican wakati wa mkutano wake uliofanyika katika mji wa Cleveland, Marekani.

Vyanzo vya habari vimedai kwamba mchezaji wa kikapu, LeBron James pamoja na meneja wa Bieber, Scooter Braun ni watu waliomshawishi aikatae ofa hiyo.

James alimkataza Bieber kutumbuiza huku Braun akimtishia kujiondoa kama meneja wake iwapo angekubali ofa hiyo ya kutumbuiza katika mkutano wa Chama hicho ambapo mgombea wake urais ni Donald Trump.

CAA, kampuni inayomwakilisha Bieber, ilipokea ofa hiyo ya kutumbuiza kwa dakika 45 kwenye ukumbi karibu na Quicken Loans Arena, ambako mkutano mkuu wa Republican ulipofanyika.

Mapromota walidai kuwa show hiyo haikuwa ya kisiasa, kiasi hicho cha fedha kilichangwa na wadhamini wa chama hicho kwa ajilili ya mwanamuziki huyo kutumbuiza.

Kiasi hicho cha fedha ni kikubwa ambapo malipo yangekuwa makubwa zaidi ya mara moja kwa Bieber kupewa katika maisha yake ya muziki au kikubwa zaidi kwa msanii kuwahi kupewa mara moja.

Staa huyo hapo awali alifikiria kutumbuiza kutokana na kuwa na asili na Canada na kwamba siasa ya Marekani hazimhusu.

Hata hivyo meneja wake ni shabiki mkubwa wa mgombea Urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na pia mmoja wa wachangishaji fedha katika chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *