Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake kinaweza kushinda ligi msimu huu baada ya bahati mbaya ya msimu uliopita.

Liverpool ilianza msimu wa 2016-17 vizuri na walikuwa pointi sita pekee nyuma ya viongozi na hatimaye bingwa wa ligi Chelsea mnamo mwezi Januari.

Lakini walirudi nyuma baada ya kupata ushindi mmoja mwezi Januari na Februari kabla ya kumaliza katika nafasi ya nne pointi 17 nyuma ya Chelsea.

”Tutashiriki mechi za ubingwa.hatutaki kuanza msimu bila kuwa na lengo lolote”, alisema Klopp.

“Lazima tuwe na lengo na nadhani tuna timu nzuri sana sasa.tulikuwa na bahati mbaya msimu uliopita”.

”Nadhani tunaweza kucheza vyema .Tuwe na matumaini kwamba kila kitu kitakuwa shwari. Klop alisema kuwa kwamba mchezaji Phillipe Coutinho hauzwi, licha ya Barcelona kumtaka”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *