Timu ya taifa ya Marekani imemtimua kocha wake Jurgen Klinsmann baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo hivi karibuni.

Klinsmann mwenye miaka 52 aliyeshinda kombe la dunia akiwa mchezaji mwaka 1990 alianza kukinoa kikosi cha Marekani mwaka 2011.

Kocha huyo Klinsmann alifanikiwa kuifikisha Marekani hatua ya 16 katika michuano ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.

Katika mechi za hivi karibuni za kufuzu kombe la dunia walifungwa goli 2-1dhidi ya Mexico na baadae kufungwa 4-0 na Costa Rica katika hatua ya kufuzu kombe la dunia.

Kwa matokeo hayo yanifanya Marekani kubakia mkiani mwa timu sita ikiwa haina alama yoyote hadi sasa.

Klinsmann mshambuliaji wa zamani wa Tottenham alihusishwa kuinoa timu ya taifa ya England baada ya Sam Allardyce kubwaga manyanga mwezi Septemba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *