Wanamuziki wa Bongo fleva, Juma Nature na Peter Msechu wanatarajia kutoa burudani kwenye tamasha la  sanaa (Siku ya msanii) litakalofanyika katika viwanja vya Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam hapo kesho.

Wanamuziki hao wataungana na wasanii wengine wa kazi mbali mbali za sanaa kwa ajili ya kutoa burudani siku hiyo muhimu kwao ambapo kutakuwa na shughuli mbali mbali za kazi za sanaa.

Siku ya msanii ni mradi uliobuniwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ukiwa a lengo la kutambua, kuhamasisha na kuthamini kazi na mchango mkubwa unaotolewa na wasanii mbalimbali hapa nchini.

Peter Msechu
Peter Msechu

Maadhimisho ya mwaka huu kilele chake kitakuwa tarehe 29 Oktoba mwaka huu ambapo wasanii mbalimbali watapewa tuzo baada ya kupitia mchujo wa kitaaluma na vigezo vilivyowekwa.

Tamasha hilo la siku ya msanii imeanza kuadhimishwa rasmi hapa nchini kuanzia mwaka 2014 na mpaka sasa linaendelea kila mwaka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *