Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Juma Kasimu “Nature” amesema kwamba yupo tayari kumpokea aliyekuwa member mwenzake katika kundi la TMK Wanaume Halisi, KR Mullah kama atakubali kurudi.

Kauli hiyo ya Nature inakuja kufuatia kusambaa kwa picha zikimuonesha KR Mulla akiwa amelala huku ajitambui maeneo ya barabarani baada ya kutundika mtungi kupita kiasi.

Nature ambaye alikuwa msanii wa kwanza kutuma picha zile kwenye ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa alitumiwa picha zile na kuambiwa amsaidie ndugu yake ambaye ni KR Mullah.

Nature aliongeza kwa kusema alichokunywa zile siyo pombe bali ni sembee mtu huwezi kunywa bia hivyo hadi ukalale kwenye mtaro kuanzia asubuhi mpaka saa 6” na pia Nature alimaliza kwa kusema akirudi TMK atampokea kwa sababu bado anampenda kama ndugu yake na milango iko wazi.

KR Mulla
KR Mulla

Kwa upande wake KR baada ya kusikia kauli hiyo ya Nature alijibu kwa kusema kama Nature angekuwa anataka kumsaidia basi asingeweza kwenda kulalama kwenye mitandao ya kijamii.

KR amesema kwamba amesikia Nature kama analalama kwenye mitandao lakini adhani kama angekuwa ananimpenda angekuwa anamsema vibaya kuwa anatumia madawa ya kulevya.

KR Mulla kwasasa amejiunga kundi la Rada Entertainment linaloongoza na TID mnyama baada ya kutoka TMK Wanaume Halisi chini ya Juma Nature.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *