Msanii nguli wa bongo fleva , Juma Nature amesema kwamba anavutiwa sana na mwanamuziki nyota wa Nigeria, Yemi Alade kutokana na juhudi zake anazozionesha kwenye muziki.

Juma Nature amesema anampenda sana mwanamuziki huyo kutokana na juhudi zake kwenye kazi na kujiheshimu kwake ndiyo kunamfanya staa huyo amkubali sana.

Msanii huyo aliendelea kwa kusema anatamani angepata nafasi ya kufanya kazi na mwanamuziki huyo kutokana na kujua muziki kwa kiasi kikubwa sana.

Yemi Alade
Yemi Alade

Nature aliendelea kusema kwamba nyimbo zake amezipenda na ingetokea siku akafanya naye nyimbo angefurahi sana.

Yemi Alade ni miongoni mwa wanamuziki wanaofanya vizuri kwasasa ndani ya Nigeria na nje kwani ameshafanya kazi na wasanii kibao wa Afrika kama Diamond Platnumz pamoja na Sauti Soul kutoka Kenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *