Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Nature amekanusha kulipwa na Harmorapa kwenye wimbo wa ‘Kiboko ya mabishoo’ na kudai kuwa hana pesa za kumlipa.

Nature amesema kwamba alikubali kushiriki katika wimbo huo kwa sababu anaamini msanii huyo chipukizi ana uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuamini atafika mbali.

 Nature  amesema yeye ameshakuwa mkongwe hivyo vijana kama Harmorapa wanapotokea kwenye ‘game’ inamlazimu kutoa sapoti ili hata watakapoondoka kuwe na watu wa kuendeleza muziki.

Nature amesikitika kusikia taarifa ambazo Harmorapa alidai kuwa amemlipa Nature kwa kolabo na kuongeza hizo taarifa kwa upande wake hazimkufikia rasmi.

Harmorapa aliwahi kunukuliwa akisema siyo busara kwa wasanii wakongwe kuwalipisha pesa wasanii wachanga kwa kuwa ndiyo kwanza wanaanza kutafuta pa kutokea na kuweka wazi kuwa kwa upande wake alilazimika kumnunulia nguo Nature za kufanyia video ya ‘Kiboko ya Mabishoo’.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *