Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Juma Nature amewataka wasanii wachanga kufuata sheria pale wanapotaka kutumia nyimbo za wasanii wakongwe jukwaani.

Kauli hiyo ya Juma Nature imekuja kufuatia hivi karibuni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy kuingia katika mgogoro na msanii mkongwe Ray C baada ya kutumia nyimbo zake wakati akiwa kwenye tamasha la Fiesta linaloendelea nchini.

Juma Nature amesema kuwa inatakiwa wasanii hao waombe kibali kwa muhusika na ikiwezekana amlipe fedha ili aimbe nyimbo zake na si kujiamulia tu kuimba.

Msanii huyo aliyetamba akiwa na TMK Wanaume Family amesema kuwa msanii mchanga kuimba nyimbo za msanii mkongwe jukwaani sio jambo baya na inaonyesha heshima lakini ni vyema wakawa na makubalino maalum kabla hajafanya hivyo kuepusha migogoro.

Wasanii wachanga wamekuwa wakitumia nyimbo za wakongwe wa Bongo Fleva wakati wa matamasha yao jambo ambalo lilionekana kama heshima kwa wakongwe hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *