Staa mkongwe wa Bongo fleva, Juma Nature amefunguka kwa kusema kuwa kuna baadhi ya watu wanahonga katika vituo vya redio nchini ili nyimbo zake za TMK Wanaume Halisi zisipigwe katika vituo hivyo.

Nature amedai kuwa kuna watu wanahonga ili nyimbo zake na za TMK Halisi zisichezwe redioni ili kumkwamisha.

Staa huyo mkongwe aliyewahi kutamba na nyimbo kama vile ‘Hili Game’ ‘Jinsi Kijana’ na ‘Hakuna Kulala’ na nyingine kibao amesema kuwa miongoni mwa watu hao wanaohonga ili nimbo zake zisipigwe ni uongozi wake wa zamani lakini hakuwa tayari kuwataja kwa majina.

Nature alikuwa akifanya kazi chini ya kundi la Wanaume Family kundi linalomilikiwa na Said Fella kabla ya kujitoa kwenye kundi na baadhi ya wasanii wengine waliokuwa kwenye kundi hilo na kuanzisha kundi lao jipya linalofahamika kama Wanaume Halisi.

Ukizungungumzia historia ya muziki wa Bongo Flava, haiwezi kukamilika bila kulitaja jina la  Juma Nature kutokana na mchango wake kwenye muziki huo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *