Mrembo, Julitha Kabete amechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo wa dunia Miss World 2017 yatakayofanyika nchini China.

Baada ya kukabidhiwa bendera mrembo huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Hi everyone, I’m honored to be representing my beautiful country Tanzania in Miss World this year…… I am humbled to carry the Tanzanian flag higher to the world. Together with support I belive we can. Wish me Luck and prayers ??. ????????

Watanzania wenzangu, kwa heshima na taadhima ninayo furaha kuiwakilisha nchi yangu kwenye mashindano ya kimataifa ya urembo ya dunia ‘Miss World’ Hii ni heshima kubwa sana kwangu, kwa familia yangu na kwa taifa langu. Ninshukuru Mungu kwa kwa nafasi hii ya kipekee. Kwa maombi na sapoti ya watanzania Nina hakika nitaweza kuiinua juu Bendera yetu na kuliwakilisha vyama taifa letu la Tanzania?? ……Mungu ibariki Tanzania??,” ameandika mrembo huyo katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Warembo kutoka nchi 120 wanatarajiwa kushiriki shindano hilo ifikapo Novemba 18 mwaka huu nchini China katika ukumbi wa Sanya City Arena. Kituo cha E! na Phoenix TV, ndiyo wataoorusha matangazo mubashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *