Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kiwelu ‘Julio’ ametangaza kuachana na soka kutokana na uamuzi mbovu wa marefa hapa nchini.

 Julio alitangza uamuzi huo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wake dhidi ya Mbeya City ulifanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Mwadui FC kufungwa goli 1-0.

Julio baada ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya alitangaza kuachana na soka la Tanzania, hiyo inatokana na kutoendelea kuridhishwa na uwezo wa waamuzi wa soka wa Tanzania, kwani katika mchezo dhidi ya Mbeya City amekiri kuwa walifungwa kihalali lakini muamuzi alionesha kuwawekea vikwazo wasisawazishe.

Kocha huyo ambaye ni mcehzaji wa zamani wa Tanzania pia amewahi kuifundisha Simba SC amekasarishwa na uamuzi uliofanywa katika mechi hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *